Saturday, 7 September 2019

Kwa mahitaji ya uyoga fresh kutoka shamba weka oda yako sasa na jinsi ya kuupata tuachie sisi.
Wasiliana nasi 0783182632. Whatsup 0757315931. E-mail orders@hertufarms.co.tz

#HertuMushrooms
#FreshnNatural

Wednesday, 17 January 2018

#MabadilikoniLazima
Hertu Farms Temise Tanzania tunaamini sekta ya Uyoga licha ya kutopewa umuhimu mkubwa hapa nchini, ni sekta muhimu sana kwa watanzania kwani unagusa mambo makubwa matatu muhimu katika jamii ambayo ni Afya, Uchumi na Mazingira.
Huu ni msukumo mkubwa kwetu unaofanya usiku na mchana kupambana tukiamini licha ya kuwa ni biashara lakini tunagusa maisha ya jamii;. kwa uchache uyoga kiafya una viinilishe vinavyoimarisha na kukinga miili yetu dhidi ya magonjwa mbalimbali, Ki-uchumi; uyoga ni biashara nzuri ya kuingiza kipato kwa jamii na mwisho uyoga ni njia mojawapo ya kutunza mazingira kutokana na utumiaji wa takataka mbalimbali (hasa masalia mbalimbali ya mazao) kuzalishia uyoga.
Kwa mahitaji ya Uyoga, Mbegu bora Uyoga, Mafunzo na Ushauri elekezi (uanzishwaji wa miradi ya kilimo cha Uyoga) wasiliana nasi kupitia kurasa zetu au simu 0713600915 au 0783182632.
Karibu sana!
Pichani mavuno ya Uyoga shambani #HertuFarms #Kisarawe

Tuesday, 24 October 2017

#MabadilikoniLazima
Tunashukuru #Mufindi na hasa Dada #Mary na familia yake, tumehitmisha uanzishwaji wa mradi wa Kilimo cha Uyoga kibiashara, tumetoa mafunzo ya Ujasiliamali/Ufanyaji Biashara, Masoko, uzalishaji Uyoga kibiashara, tukajenga banda/Shamba tutakaanda udongo wa kuoteshea uyoga(kimeng'nywa) na hatimaye kupanda uyoga kitaalamu chini ya uangalizi wetu. Tunaamini kupitia Dada #Mary #Mufindi na mkoa wa #Iringa kwa ujumla watahamasika kuchangamkia fursa ya kilimo cha Uyoga ili kujikwamua na umaskini na zaidi kuimarisha afya zao.
#MabadilikoniLazima
UYOGA NA MAZINGIRA
Kilimo cha uyoga ni njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira yetu;
1.Hulimwa kwa kutumia masalia mbalimbali ya mazao kama; maranda ya mbao (malaini-saw dust na magumu), Maganda-ya alizeti, karanga,miwa,maharage nk. Majani-mpunga,mikunde,ngano, magugu maji nk, magunzi ya mahindi mabua ya mahindi,mtama n.k hii hupunguza uchafu ambao ungetupwa au kuchomwa na kuchafua mazingira
2. Baada ya kumalizwa/kukoma kuvunwa masalia ya kimeng'enywa hutumika kama mbolea nzuri (kwa kilimo hai) kwa ajili ya mazao mbalimbali hasa bistani ya mboga mboga ,pia masalia hayo hutumika kwa ajili ya kulishia wanyama mbalimbali.
Kwa mahitaji ya Uyoga, bidhaa za Uyoga kama Sambusa, Unga, n.k pia mafunzo ya kuzalisha Uyoga kibiashara, wasiliana nasi 0713600915 au 0783182632
#KilimochaUyoga
#KilimoHai
#UyogakwaAfya



Wednesday, 9 August 2017


Taasisi za HERTU Investment na Tanzania Enterpreneurs Motivation in Self Employment (TEMISE) chini ya mradi ujulikanao kama Hertu Farms, (zinaojihusisha na mafunzo ya ujasiliamali, uendelezaji biashara na  kilimo biashara ikiwemo kilimo cha uyoga, matunda, mboga mboga na ufugaji wa kuku wa kienyeji) zimeendesha mafunzo ya Biashara, masoko, utoaji huduma bora kwa wateja pamoja na kilimo cha uyoga kibiashara, yenye lengo la kuwajengea uwezo wakinamama ili waweze kuboresha biashara zao na  kuzalisha uyoga kibiashara ili waweze kuboresha vipato vyao na hasa kupunguza umaskini.
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyohusisha nadharia na vitendo yalifanyika kuanzia tarehe 6/8/2017 na kumalizika tarehe 9/8/2017, yalifanyika katika kijiji cha Mwanzo Mgumu, Wilaya ya kisarawe, Mkoa wa Pwani. Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo,  ndugu Herman Msagamasi  kutoka HERTU Investment  amesema kuwa utoaji wa mafunzo hayo ni utaratibu waliojiwekea  ambapo kila mwezi hutoa nafasi kwa jamii kujifunza kile taasisi hizo zinafanya, ambapo safari hii waliamua wawajengee uwezo akina mama mbalimbali katika nyanja za Biashara,Masoko,  utoaji wa huduma bora kwa wateja; wakitambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Biashara na hasa namna bora ya kutafuta masoko na kuyahudumia ipasavyo, kwa kutoa huduma bora; pia mafunzo yaliangaziazia kuwafanya wakina mama kuacha kufanya biashara zao kimazoea kama kutoweka kumbukumbu, kutohudumia wateja ipasavyo, kusubiri wateja wawafuate n.k. Pia Mafunzo yalilenga kuwafundisha wakina mama kuzalisha uyoga kama zao la chakula na Biashara; kwa kuzingatia kuwa sekta hii  ya Kilimo cha Uyoga inakuwa kwa kasi nchini ingawa bado hakijapewa umuhimu mkubwa licha ya faida kubwa kiafya, kuingiza kipato na utunzaji wa mazingira.
Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo Ndugu Shaban Kabanga kutoka TEMISE amesema, wajasiliamali wengi wamekuwa wakifanya biashara kwa mazoea na kupelekea kutofikia malengo yao hivyo kupelekea kupoteza muda na rasilimali zao; ameongeza kuwa wajasiliamali wengi wamekuwa wanawekeza kwenye miradi kwa mkumbo, bila ya kufanya utafiti wa kina; anaamini kuwa mafunzo waliyopewa wakina mama hao yatawawezesha  kufanya kufanya ujasilimali mbalimbali kwa ufanisi mkubwa na pia kuzalisha uyoga  kibiashara; ameongeza kuwa; wakina mama  hawajapewa mafunzo ya kuzalisha uyoga pekee kama wanavyofanya wengi bali wamepewa na mbinu za namna ya kufanya Biashara ya kilimo cha uyoga kwa kuzalisha uyoga bora, kufungasha vyema, kupanua wigo wa masoko, na kuhudumia vizuri wateja wao ili kujenga soko kubwa hivyo biashara zao kuwa endelevu. Kwa upande wa washiriki w mafunzo hayo;  Bi. Anna mmoja wa washiriki amesifu namna mafunzo yalivyotolewa kwa kutumia vitendo zaidi kuliko nadharia hivyo imemfanya aelewe zaidi na anaamini  itamsaidia katika kuutekeleza ipasavyo miradi yake na hasa kuanza kilimo cha uyoga. Nae Bi. Sarah akizungumzia mafunzo hayo amesema yamemjenga vilivyo kwani zamani alikuwa anafanya biashara kimazoea mpaka kupelekea kufirisika na kuwa na madeni makubwa;  hivyo kupitia mafunzo hayo amefahamu kosa lake na ataweza kujirekebisha; "pia nimejifunza uyoga ni chakula bora sana kuboresha afya zetu kwa kuwa una viinilishe vingi na ni biashara nzuri sana kwani kilimo chake ni rahisi kwa mtaji, eneo dogo, maji kiasi na huchukua muda mfupi hadi kuvuna na pia unavunwa kipindi chote cha mwaka kwani hautegemei mvua. 
Kwa mujibu wa taasisi hizo, mafunzo kama hayo yanatarajia kufanyika tena tarehe 18.08.2017, jijini Dar es salaam.

Thursday, 3 August 2017




Tumekuwa tukiulizwa na watu wengi sana juu ya soko la uyoga nchini Tanzania. Makala hii inajikita kuelezea hali halisi ya soko la uyoga na biashara kwa ujumla.
Uyoga na mazao yake (bahati mbaya hadi sasa tunazalisha uyoga pekee)  licha ya kuwa na faida kubwa kwa nchi na kwa kipato cha mwanachi mmomoja.Kilimo na  biashara ya uyoga katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ipo chini sana. Kilimo kinafanyika kwa uchahe sana na kiasi kidogo; kwa maana ya kilimo kinafanyika si kibiashara hivyo kutokuleta tija kwa taifa na kwa wakulima.

Soko la uyoga
Je, Uyoga una soko?    Kilimo cha Uyoga kinalipa?
Awali ya yote bidhaa yoyote ili iweze kupata soko, ari, bidii na juhudi kubwa inabidi kufanyika kuanzia katika kuizalisha ili iwe  bora na inayopendwa na wateja;  pia katika kuitengenezea mazingira mazuri ya ya bidhaa hiyo kununulika kama  kuitangaza n.k

Tunasema uyoga una soko kubwa hasa hapa nchini na ni biashara kubwa. Zifuatazo ni hoja kadhaa zinazothibitisha hoja hii.

·     1. Uyoga ni utamaduni wa Mtanzania: Uyoga tangu enzi umekuwa ukitumika kama chakula na dawa kwenye makabila mengi hapa nchini Tanzania. Makabila mengi kipindi cha masika wamekuwa wakivuna uyoga porini  na kuutumia kama mboga au kutibu magonjwa mbalimbali; pia uyoga hukaushwa na kutunzwa kwa matumizi ya baadae. Uvunaji au ukusanyaji wa uyoga huu hukabiliwa na changamoto kadhaa kama; 

(a)  uyoga hupatikana kipindi cha mvua (masika) pekee
(b)  kushambuliwa kwa wavunaji na wadudu au wanyama wakali kama nyoka n.k,
(c)  kuvuna/kukusanya uyoga wenye sumu kimakosa (kuna uyoga unaofaa kuliwa na wenye sumu ambao haufai kuliwa na mwanadamu).
(d)  uharibifu wa mazingira; kuna mahusiano makubwa baina ya uyoga na mazingira endapo; mazingira hayatatunzwa ipasavyo uyoga hautamea/hautapatikana. Hivi sasa uyoga haupatikani kwa wingi kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Hii hoja inadhihirisha kuwa kilimo cha uyoga ni fursa kubwa nchini, uwepo wa teknolojia ya kulima Uyoga inafanya Uyoga upatikane kipindi chote cha mwaka (na kama tafiti zikifanyika kwa wingi aina nyingi za uyoga kutoka porini zitalimwa kwenye mashamba ya uyoga), kupunguza vifo vitokanavyo na ulaji wa uyoga sumu au kushambuliwa na wanyama, na pia kusaidia utunzaji wa mazingira. Endapo wakulima watalima uyoga kibiashara; uyoga ni biashara kubwa na itawezesha kuongeza pato la taifa na kuwa chanzo cha ajira nchini.

2  2. Kubadilika kwa mtindo wa maisha  : kumekuwa na uhamiaji mkubwa wa watu kutoka vijijini kwenda mjini; hii imesababisha ile ari na mwamko wa ulaji wa uyoga kupungua kwani licha ya kuwa na mtu anauhitaji mkubwa kwani alikuwa anaula alipokuwa kijijini. Hii imesababishwa na kutopatikana kwa urahisi uyoga maeneo ya mijini, mtu akihitaji uyoga ni lazima aagize uyoga vijijini. Kutokana na mwamko wa ulaji wa uyoga kushuka imepelekea kizazi kinachofuatia pia kutokuwa na ari na mwamko wa kula uyoga licha ya faida zinazopatikana mwilini.
Mtindo wa maisha  ni pamoja na ulaji, ulaji kwa miaka ya hivi karibuni umebadilika kutokana na sababu mbalimbali  watu sasa wameacha au kupunguza  kula vyakula vya asili na kupendelea kula vyakula vya kisasa.

·      3. kuwepo kwa wageni kutoka nchi mbalimbali; baadhi ya nchi ulaji wa uyoga ni utamaduni unaoendelezwa, kutokana na faida za kilishe zinazopatikana kwenye uyoga, hivyo wanapokuwa hapa nchini hupendelea kuendelea na utamaduni wao. Kumekuwa na migahawa mingi nchini inayopika vyakula mahsusi kutokana na utamaduni wa taifa fulani, mfano migaawa ya kichina, kifaransa, kijerumani n.k
·          Uwepo wa mahoteli, migahawa (restaurants), maduka makubwa ya vyakula na vitu vingine (supermarkets); hoteli na maduka makubwa ni sehemu zenye uhitaji mkubwa wa bidhaa hasa za kilimo na Uyoga ukiwemo.

·       4. itaji mkubwa wa uyoga unaolimwa au kupatikana ukanda wa afrika; mataifa mbalimbali ya ulaya yanaamini nchi zinazoendelea hasa za afrika bado mazingira hayajachafuliwa sana kulinganisha na nchi zao. Hivyo mataifa hayo hupendelea bidhaa nyingi hasa za kilimo ukiwemo uyoga kutoka ukanda wetu wan chi za kiafrika; ingawa bado uyoga haujapewa kipaumbele kama mazao mengine ya kilimo.

·      5. wamko mdogo wa kulima uyoga: Nchini Tanzania na nchi zingine za kiafrika kilimo cha uyoga bado hakijatiliwa mkazo licha ya kuwa ni na faida kubwa kiafya, kiuchumi na kimazingira. Ni wakulima wachache sana wanaojihusisha na kilimo cha Uyoga kibiashara licha ya uhitaji mkubwa wa uyoga.
·       6. Kutokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha hasa ulaji mbaya wa chakula kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo la moyo, matatizo ya figo n.k; wagonjwa wenye magonjwa hushauriwa kula uyoga. Pia kumekuwepo na mwamko mkubwa wa jamii juu ya ulaji wa vyakula vya asili (organic food) ikiwemo Uyoga hivyo ulaji na mahitaji ya Uyoga yanaongezeka siku hadi siku.
 
Mwisho:Kutokana na sababu tajwa na sababu nyingine nyingi tunathubutu kusema kuwa uyoga una soko kubwa na ni fursa mpya na yenye uwezo wa kuleta kipato kwa mkulima au mfanyabiashara wa uyoga na bidhaa zake na cha zaidi kuliingizia taifa pato kubwa. Ni sekta kubwa inayokuwa kwa kasi na endapo watanzania tutachangamkia fursa hii kwanza tutaimarisha afya za wananchi na kukuza uchumi wa nchi.
Moja ya changamoto kubwa katika kilimo cha uyoga ni upatikanaji wa Mbegu bora; kwa kuliona hilo HERTU INVESTMENT kupitia mradi wake wa HERTU Farms tunawaletea mbegu bora za Uyoga aina ya Mamama/Oyster mushrooms (nyeupe, pinki na grey), ukiweka oda baada ya siku 14 (wiki mbili) mbegu zinakuwa tayari. Bei ni Tsh. 3,000 kwa chupa.
Unaweza kupiga simu 0783182632/0713600915; Barua pepe hertufarms@yahoo.com au kwa njia ya Whatsup 0757315931

Tunasafirisha mikoa mbalimbali Tanzania na nchi jirani

Pia tunatoa Mafunzo, ushauri, uanzishaji, usimamizi na tathmini ya miradi ya kilimo cha Uyoga kibiashara.
Tunapatikana Mwananyamala-komakoma, Biashara complex, Ghorofa ya 3, Ofisi #301; pia shambani Kisarawe-Mwanzomgumu, Mkoa wa Pwani.

KARIBU KATIKA SEKTA HII MPYA INAYOKUA KWA KASI NCHINI; KWA KUIMARISHA AFYA, KIPATO NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

#MabadilikoniLazima
Pinki
Hudhurungi (Grey)
Nyeupe




 
Banda/Shamba la kuoteshea uyoga linajengwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana kwenye mazingira yako. Sehemu za joto linaweza kujengewa nyasi na udongo, matete, Makuti n.k. ili kuhifadhi ubaridi na sehemu za joto hata tofali na bati unaweza kujengewa.

SIFA ZA BANDA
1. Liwe na uwezo wa kuhifadhi unyevu nyevu na ubaridi
2. Liwe na uwezo wa kuzuia wadudu na wanyama waharibifu kama panya,jongoo,konokono, pia inzi n.k
3. Liwe na mzunguko mzuri wa hewa n mwanga wa kutosha hasa wakati wa kuotesha; isipokuwa wakati wa utandaji wa mbegu mifuko ya uyoga unahitaji giza kiasi
4. Banda lisijengwe karibu na jalala la takataka, mabanda ya wanyama kama kuku,ng'ombe n.k
4. Lisiruhusu jua kuingia na upepo mkali
5. Liwe safi muda wote.
Kwa ushauri na mafunzo juu ya #KilimochauyogaKibiashara wasiliana na wataalamu waliobobea kwa namba 0783182632/0713600915 pia unaweza kufika Mwananyamala-Komakoma, Jengo la Biashara Complex, Ghorofa ya 3,Ofisi #301.
#UyogakwaAfyaKipatoMazingira

 #MabadilikoniLazima
Tumia maarifa, vipawa, rasilimali, muda na chochote ulichonacho kuhakikisha ndoto yako inatimia, ili uweze kutathmini, kama inafaa uweze kupanua wigo wa ndoto yako; huwezi kujua kama ndoto yako ni bora au sio mpaka uifanyie kazi mpaka mwisho; usiguse jambo au biashara ya ndoto yako na kuacha kabla hakijatimia wengi tumekuwa tukitaka kufanya mengi na kuacha bila ya kukamilisha hapo unakuwa unapoteza muda na rasilimali zako na hutofanikisha ndoto zako. Fanya tafiti wa kina katika ndoto yako na ukiona ina tija itekeleze kwa nguvu zako zote mpaka itimie.


Thursday, 27 July 2017

Nchi ya viwanda inawezekana endapo wajasiliamali watakuwa wabunifu wa kuanzisha viwanda vya kutenengeza  bidhaa bora na kwa wingi au kujikita katika kuzalisha  malighafi zitakazohitajika katika  viwanda vitakavyoanzishwa.Tusisubiri kuajiriwa kwenye viwanda hivyo; si lazima kuwa na mtaji mkubwa kuanzisha kiwanda, unaweza kuanza na kidogo; sekta ya viwanda ni sekta mtambuka inayotegemea sekta nyingi ili kuendelea. Itafika muda viwanda vingi vitaanzishwa na kuhitaji malighafi nyingi kutoka nchini, endapo vwanda havitapatamalighafi ya kutosha vikianza kuagiza nje tutaanza kulalamika. Hivyo chukua hatua sasa kwa kuchangamkia fursa mbalimbali kutokana na sera hii, fanya tafiti na amua sasa!





TEMISE Tanzania na HERTU Investment tunahitaji watu wenye ujuzi, wachapakazi, wabunifu, na waaminifu watakaohusika na uuzaji na usambazaji wa bidhaa na utangazaji wa huduma zinazotolewa na taasisi. 

Tuesday, 11 July 2017

Burns Cholesterol:
As mushrooms are full of proteins, fibers, enzymes, and low carbohydrates with zero cholesterol and fats, they can keep you safe from cholesterol by burning it after digestion.

 Prevents Breast And Prostate Cancers:
Mushrooms include beta-glucans and conjugated linoleic acid with anti-carcinogens. These help in preventing breast cancer and prostate cancer. Linoleic acid helps in suppressing estrogen in women after menopause to prevent breast cancer while Beta-Glucans helps in preventing prostate cancer. Selenium helps the most in suppressing these cancerous cells.

 Perfect Diet For Diabetics:
Mushrooms contain no fat, low carbohydrates, high proteins, enzymes, vitamins, minerals, and fibers. Thus, it is an ideal diet for diabetics. The natural enzymes in it help in breaking down the sugars and starch. They also improve the functioning of the endocrinal glands. Moreover, the natural antibiotics in mushrooms help the diabetic people from easily prone infections.

 Helps Build Immunity:
The combination of vitamins A, B, and C in mushrooms help build good immune system. The strong antibiotics present in them helps to fight against infections. The antioxidant, Ergothioneine protects from free radicals.

 Aids in Weight Loss:
Everyone knows that to lose fat and cholesterol, you need to burn that extra fat which is ideally used to digest the proteins in your body. While dieting, it is always recommended to take high protein; low carbohydrates and no fat diet which is offered by mushrooms.

Vitamin D:
Mushroom is the only vegetable which contains vitamin D. It contains calcium, iron, potassium, copper, and selenium.

Vitamin B1:
Mushrooms are also a good source of Vitamin B1, which is also known as Thiamin. Thiamin is responsible for controlling the release of energy from carbohydrates. This is required for the normal functioning of our nervous system and brain.

Vitamin B2:
Mushrooms are enriched with Riboflavin or vitamin B2. This vitamin promotes good vision and eye health. Not only this, but it also maintains healthy red blood cells, which strengthens our immune system. Vitamin B2 present in mushroom is also responsible for healthy skin.

 Vitamin B3:
Niacin or Vitamin B3 is another important B-vitamin that is found in mushrooms. It helps in controlling the release of energy from carbohydrate, fat, and protein. This tends to keep our body’s nervous system and digestive system in good shape.

 Vitamin B5:
Vitamin B5, also known as Pantothenic Acid, is naturally found in mushrooms. It is a very important vitamin that is essential for various metabolic roles in our body. Pantothenic Acid also provides assistance in producing hormones in our body.

Vitamin B6:
Vitamin B6 is also found in mushrooms. It helps in boosting your mood. Vitamin B6 regulates our body’s internal clock that is very important for normal brain function and development. This vitamin is also responsible for alleviating mood swings and depression.

 Vitamin B9:
Mushrooms are very rich in vitamin B9, which is commonlycommonlyy known as Folate. Vitamin B9 helps in the formation of white blood cells and red blood cells in bone marrow. Folate is also very essential for healthy growth of the body. Even pregnant women are advised to consume Folate, which helps in the proper growth of the fetus.

 Vitamin H:
Vitamin H or Biotin is also a B-vitamin type that is found in mushrooms. It is essential in the metabolism of carbohydrates and proteins. It strengthens our inner health by increasing immunity.

Sunday, 18 June 2017


Ukulima wa uyoga ni kitega uchumi kinachoweza kumnasua Mkulima mapema kutoka kwenye u maskini;
1. Ukuaji wake ni wa haraka huchukua  takriban siku 30-40 kuanza  kuvunwa  tangu  Mbegu kupandwa. Hivyo hurudisha pesa haraka kwa mwekezaji, na baada ya kuanza kuvunwa  mkulima akitunza vizuri ataendelea  kuvuna kwa miezi 2 hadi 4, kwa mpando  mmoja
2. Huhitaji eneo dogo  la ardhi
3.Gharama za uendeshaji ni ndogo  sana haihitaji umeme, hutumia  masalia ya mazao na takataka kuzalishia  uyoga n.k (gharama kubwa hutumika kwa miundombinu ya awali kama mashamba na vifaa n.k)
4.Hautegemei misimu ya mvua; hivyo Mkulima hujipatia kipato chake kipindi chote cha mwaka tofauti na mazao mengine.
BAADA YA KUVUNA
5.Mabaki baada ya uyoga kuvunwa  hutumika kama mbolea nzuri na ya Asili kwa kuoteshea mimea kama matunda na mboga mboga; pia hutumika Kutengeneza chakula cha mifugo.

Lakini ili kuwa na kitega uchumi cha uhakika zaidi mtu  yoyote anayetaka kuwekeza kwenye sekta hii hana budi kujifunza vizuri, na kwa undani sayansi na teknlojia ya ukulima wa aina mbalimbali za Uyoga: Uyoga wenye soko la uhakika, Uyoga wenye manufaa katika kuboresha afya ya jamii.

Imetolewa katika kitabu cha "UYOGA, FAIDA ZAKE KU-AFYA, KI-UCHUMI, KI-MAZINGIRA, NA KATIKA UKULIMA WAKE"; Keto E. Mshingeni, PH.D
Profesa, Hubert Kairuki Memorial University

About our customers

About our customers

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget