Wednesday, 9 August 2017


Taasisi za HERTU Investment na Tanzania Enterpreneurs Motivation in Self Employment (TEMISE) chini ya mradi ujulikanao kama Hertu Farms, (zinaojihusisha na mafunzo ya ujasiliamali, uendelezaji biashara na  kilimo biashara ikiwemo kilimo cha uyoga, matunda, mboga mboga na ufugaji wa kuku wa kienyeji) zimeendesha mafunzo ya Biashara, masoko, utoaji huduma bora kwa wateja pamoja na kilimo cha uyoga kibiashara, yenye lengo la kuwajengea uwezo wakinamama ili waweze kuboresha biashara zao na  kuzalisha uyoga kibiashara ili waweze kuboresha vipato vyao na hasa kupunguza umaskini.
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyohusisha nadharia na vitendo yalifanyika kuanzia tarehe 6/8/2017 na kumalizika tarehe 9/8/2017, yalifanyika katika kijiji cha Mwanzo Mgumu, Wilaya ya kisarawe, Mkoa wa Pwani. Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo,  ndugu Herman Msagamasi  kutoka HERTU Investment  amesema kuwa utoaji wa mafunzo hayo ni utaratibu waliojiwekea  ambapo kila mwezi hutoa nafasi kwa jamii kujifunza kile taasisi hizo zinafanya, ambapo safari hii waliamua wawajengee uwezo akina mama mbalimbali katika nyanja za Biashara,Masoko,  utoaji wa huduma bora kwa wateja; wakitambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Biashara na hasa namna bora ya kutafuta masoko na kuyahudumia ipasavyo, kwa kutoa huduma bora; pia mafunzo yaliangaziazia kuwafanya wakina mama kuacha kufanya biashara zao kimazoea kama kutoweka kumbukumbu, kutohudumia wateja ipasavyo, kusubiri wateja wawafuate n.k. Pia Mafunzo yalilenga kuwafundisha wakina mama kuzalisha uyoga kama zao la chakula na Biashara; kwa kuzingatia kuwa sekta hii  ya Kilimo cha Uyoga inakuwa kwa kasi nchini ingawa bado hakijapewa umuhimu mkubwa licha ya faida kubwa kiafya, kuingiza kipato na utunzaji wa mazingira.
Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo Ndugu Shaban Kabanga kutoka TEMISE amesema, wajasiliamali wengi wamekuwa wakifanya biashara kwa mazoea na kupelekea kutofikia malengo yao hivyo kupelekea kupoteza muda na rasilimali zao; ameongeza kuwa wajasiliamali wengi wamekuwa wanawekeza kwenye miradi kwa mkumbo, bila ya kufanya utafiti wa kina; anaamini kuwa mafunzo waliyopewa wakina mama hao yatawawezesha  kufanya kufanya ujasilimali mbalimbali kwa ufanisi mkubwa na pia kuzalisha uyoga  kibiashara; ameongeza kuwa; wakina mama  hawajapewa mafunzo ya kuzalisha uyoga pekee kama wanavyofanya wengi bali wamepewa na mbinu za namna ya kufanya Biashara ya kilimo cha uyoga kwa kuzalisha uyoga bora, kufungasha vyema, kupanua wigo wa masoko, na kuhudumia vizuri wateja wao ili kujenga soko kubwa hivyo biashara zao kuwa endelevu. Kwa upande wa washiriki w mafunzo hayo;  Bi. Anna mmoja wa washiriki amesifu namna mafunzo yalivyotolewa kwa kutumia vitendo zaidi kuliko nadharia hivyo imemfanya aelewe zaidi na anaamini  itamsaidia katika kuutekeleza ipasavyo miradi yake na hasa kuanza kilimo cha uyoga. Nae Bi. Sarah akizungumzia mafunzo hayo amesema yamemjenga vilivyo kwani zamani alikuwa anafanya biashara kimazoea mpaka kupelekea kufirisika na kuwa na madeni makubwa;  hivyo kupitia mafunzo hayo amefahamu kosa lake na ataweza kujirekebisha; "pia nimejifunza uyoga ni chakula bora sana kuboresha afya zetu kwa kuwa una viinilishe vingi na ni biashara nzuri sana kwani kilimo chake ni rahisi kwa mtaji, eneo dogo, maji kiasi na huchukua muda mfupi hadi kuvuna na pia unavunwa kipindi chote cha mwaka kwani hautegemei mvua. 
Kwa mujibu wa taasisi hizo, mafunzo kama hayo yanatarajia kufanyika tena tarehe 18.08.2017, jijini Dar es salaam.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

About our customers

About our customers

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget