Sunday, 18 June 2017


Ukulima wa uyoga ni kitega uchumi kinachoweza kumnasua Mkulima mapema kutoka kwenye u maskini;
1. Ukuaji wake ni wa haraka huchukua  takriban siku 30-40 kuanza  kuvunwa  tangu  Mbegu kupandwa. Hivyo hurudisha pesa haraka kwa mwekezaji, na baada ya kuanza kuvunwa  mkulima akitunza vizuri ataendelea  kuvuna kwa miezi 2 hadi 4, kwa mpando  mmoja
2. Huhitaji eneo dogo  la ardhi
3.Gharama za uendeshaji ni ndogo  sana haihitaji umeme, hutumia  masalia ya mazao na takataka kuzalishia  uyoga n.k (gharama kubwa hutumika kwa miundombinu ya awali kama mashamba na vifaa n.k)
4.Hautegemei misimu ya mvua; hivyo Mkulima hujipatia kipato chake kipindi chote cha mwaka tofauti na mazao mengine.
BAADA YA KUVUNA
5.Mabaki baada ya uyoga kuvunwa  hutumika kama mbolea nzuri na ya Asili kwa kuoteshea mimea kama matunda na mboga mboga; pia hutumika Kutengeneza chakula cha mifugo.

Lakini ili kuwa na kitega uchumi cha uhakika zaidi mtu  yoyote anayetaka kuwekeza kwenye sekta hii hana budi kujifunza vizuri, na kwa undani sayansi na teknlojia ya ukulima wa aina mbalimbali za Uyoga: Uyoga wenye soko la uhakika, Uyoga wenye manufaa katika kuboresha afya ya jamii.

Imetolewa katika kitabu cha "UYOGA, FAIDA ZAKE KU-AFYA, KI-UCHUMI, KI-MAZINGIRA, NA KATIKA UKULIMA WAKE"; Keto E. Mshingeni, PH.D
Profesa, Hubert Kairuki Memorial University

Related Posts:

  • SIKU YA MAMA DUNIANIKatika kuadhimisha siku muhimu ya  Mama Duniani (Mother's Day) HERTU Investment/ Hertu Farms na Temise Tanzania ambao moja ya malengo yao wamejikita katika kumkomboa mwanamke hasa kiuchumi, tukiamini kuwa mwanamke kumili… Read More
  • GANODERMA-MEDICINAL MUSHROOM Ganoderma lucidum are known as reishi in Japan and lingzhi in China. These medicinal mushrooms, which are usually ground up and added to teas and soups or sold in capsule form, have significant health benefits. Reishi mu… Read More
  • HEALTH BENEFITS OF MUSHROOMS POWDER Burns Cholesterol: As mushrooms are full of proteins, fibers, enzymes, and low carbohydrates with zero cholesterol and fats, they can keep you safe from cholesterol by burning it after digestion.  Prevents Breast And P… Read More
  • HERTU INVESTMENT/Hertu Farms na TEMISE Tanzania tunapenda kuwatangazia wajasiliamali au vikundi vinavyopenda kuanzisha mradi wa uzalishaji Uyoga kibiashara sekta ambayo inayokuwa kwa kasi nchini baada ya kuwa na umuhimu m… Read More
  • UYOGA: KITEGA UCHUMI KWA WABUNIFU WENYE BIDII Ukulima wa uyoga ni kitega uchumi kinachoweza kumnasua Mkulima mapema kutoka kwenye u maskini; 1. Ukuaji wake ni wa haraka huchukua  takriban siku 30-40 kuanza  kuvunwa  tangu  Mbegu kupandwa. Hivyo hurud… Read More

0 comments:

Post a Comment

About our customers

About our customers

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget