Uyoga na mazao yake (bahati mbaya hadi sasa tunazalisha uyoga pekee) licha ya kuwa na faida kubwa kwa nchi na kwa kipato cha mwanachi mmomoja.Kilimo na biashara ya uyoga katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ipo chini sana. Kilimo kinafanyika kwa uchahe sana na kiasi kidogo; kwa maana ya kilimo kinafanyika si kibiashara hivyo kutokuleta tija kwa taifa na kwa wakulima.
Soko la uyoga
Je,
Uyoga una soko? Kilimo cha Uyoga
kinalipa?
Awali
ya yote bidhaa yoyote ili iweze kupata soko, ari, bidii na juhudi kubwa inabidi
kufanyika kuanzia katika kuizalisha ili iwe
bora na inayopendwa na wateja;
pia katika kuitengenezea mazingira mazuri ya ya bidhaa hiyo kununulika
kama kuitangaza n.k
Tunasema
uyoga una soko kubwa hasa hapa nchini na ni biashara kubwa. Zifuatazo ni hoja
kadhaa zinazothibitisha hoja hii.
· 1. Uyoga ni utamaduni
wa Mtanzania: Uyoga tangu enzi umekuwa ukitumika kama chakula na dawa kwenye
makabila mengi hapa nchini Tanzania. Makabila mengi kipindi cha masika wamekuwa
wakivuna uyoga porini na kuutumia kama
mboga au kutibu magonjwa mbalimbali; pia uyoga hukaushwa na kutunzwa kwa
matumizi ya baadae. Uvunaji au ukusanyaji wa uyoga huu hukabiliwa na changamoto
kadhaa kama;
(a) uyoga hupatikana kipindi cha mvua (masika) pekee
(b) kushambuliwa kwa wavunaji na wadudu au wanyama
wakali kama nyoka n.k,
(c) kuvuna/kukusanya uyoga wenye sumu kimakosa (kuna
uyoga unaofaa kuliwa na wenye sumu ambao haufai kuliwa na mwanadamu).
(d) uharibifu wa mazingira; kuna mahusiano makubwa baina
ya uyoga na mazingira endapo; mazingira hayatatunzwa ipasavyo uyoga
hautamea/hautapatikana. Hivi sasa uyoga haupatikani kwa wingi kutokana na
uchafuzi wa mazingira.
Hii hoja inadhihirisha kuwa kilimo cha uyoga ni
fursa kubwa nchini, uwepo wa teknolojia ya kulima Uyoga inafanya Uyoga
upatikane kipindi chote cha mwaka (na kama tafiti zikifanyika kwa wingi aina
nyingi za uyoga kutoka porini zitalimwa kwenye mashamba ya uyoga), kupunguza
vifo vitokanavyo na ulaji wa uyoga sumu au kushambuliwa na wanyama, na pia
kusaidia utunzaji wa mazingira. Endapo wakulima watalima uyoga kibiashara;
uyoga ni biashara kubwa na itawezesha kuongeza pato la taifa na kuwa chanzo cha
ajira nchini.
2 2. Kubadilika kwa
mtindo wa maisha : kumekuwa na uhamiaji
mkubwa wa watu kutoka vijijini kwenda mjini; hii imesababisha ile ari na mwamko
wa ulaji wa uyoga kupungua kwani licha ya kuwa na mtu anauhitaji mkubwa kwani
alikuwa anaula alipokuwa kijijini. Hii imesababishwa na kutopatikana kwa
urahisi uyoga maeneo ya mijini, mtu akihitaji uyoga ni lazima aagize uyoga
vijijini. Kutokana na mwamko wa ulaji wa uyoga kushuka imepelekea kizazi
kinachofuatia pia kutokuwa na ari na mwamko wa kula uyoga licha ya faida
zinazopatikana mwilini.
Mtindo wa maisha
ni pamoja na ulaji, ulaji kwa miaka ya hivi karibuni umebadilika
kutokana na sababu mbalimbali watu sasa
wameacha au kupunguza kula vyakula vya
asili na kupendelea kula vyakula vya kisasa.
· 3. kuwepo kwa wageni
kutoka nchi mbalimbali; baadhi ya nchi ulaji wa uyoga ni utamaduni
unaoendelezwa, kutokana na faida za kilishe zinazopatikana kwenye uyoga, hivyo
wanapokuwa hapa nchini hupendelea kuendelea na utamaduni wao. Kumekuwa na
migahawa mingi nchini inayopika vyakula mahsusi kutokana na utamaduni wa taifa
fulani, mfano migaawa ya kichina, kifaransa, kijerumani n.k
·
Uwepo wa mahoteli, migahawa (restaurants),
maduka makubwa ya vyakula na vitu vingine (supermarkets); hoteli na maduka
makubwa ni sehemu zenye uhitaji mkubwa wa bidhaa hasa za kilimo na Uyoga
ukiwemo.
· 4. itaji mkubwa wa
uyoga unaolimwa au kupatikana ukanda wa afrika; mataifa mbalimbali ya ulaya yanaamini
nchi zinazoendelea hasa za afrika bado mazingira hayajachafuliwa sana
kulinganisha na nchi zao. Hivyo mataifa hayo hupendelea bidhaa nyingi hasa za
kilimo ukiwemo uyoga kutoka ukanda wetu wan chi za kiafrika; ingawa bado uyoga
haujapewa kipaumbele kama mazao mengine ya kilimo.
· 5. wamko mdogo wa
kulima uyoga: Nchini Tanzania na nchi zingine za kiafrika kilimo cha uyoga bado
hakijatiliwa mkazo licha ya kuwa ni na faida kubwa kiafya, kiuchumi na
kimazingira. Ni wakulima wachache sana wanaojihusisha na kilimo cha Uyoga
kibiashara licha ya uhitaji mkubwa wa uyoga.
· 6. Kutokana na
mabadiliko ya mitindo ya maisha hasa ulaji mbaya wa chakula kumekuwepo na
ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo la moyo,
matatizo ya figo n.k; wagonjwa wenye magonjwa hushauriwa kula uyoga. Pia
kumekuwepo na mwamko mkubwa wa jamii juu ya ulaji wa vyakula vya asili (organic
food) ikiwemo Uyoga hivyo ulaji na mahitaji ya Uyoga yanaongezeka siku hadi
siku.
Mwisho:Kutokana na sababu tajwa na sababu nyingine nyingi tunathubutu kusema kuwa uyoga una soko kubwa na ni fursa mpya na yenye uwezo wa kuleta kipato kwa mkulima au mfanyabiashara wa uyoga na bidhaa zake na cha zaidi kuliingizia taifa pato kubwa. Ni sekta kubwa inayokuwa kwa kasi na endapo watanzania tutachangamkia fursa hii kwanza tutaimarisha afya za wananchi na kukuza uchumi wa nchi.
0 comments:
Post a Comment