Nchi ya viwanda inawezekana endapo wajasiliamali watakuwa wabunifu wa kuanzisha viwanda vya kutenengeza bidhaa bora na kwa wingi au kujikita katika kuzalisha malighafi zitakazohitajika katika viwanda vitakavyoanzishwa.Tusisubiri kuajiriwa kwenye viwanda hivyo; si lazima kuwa na mtaji mkubwa kuanzisha kiwanda, unaweza kuanza na kidogo; sekta ya viwanda ni sekta mtambuka inayotegemea sekta nyingi ili kuendelea. Itafika muda viwanda vingi vitaanzishwa na kuhitaji malighafi nyingi kutoka nchini, endapo vwanda havitapatamalighafi ya kutosha vikianza kuagiza nje tutaanza kulalamika. Hivyo chukua hatua sasa kwa kuchangamkia fursa mbalimbali kutokana na sera hii, fanya tafiti na amua sasa!
Thursday, 27 July 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment