Wednesday, 9 August 2017


Taasisi za HERTU Investment na Tanzania Enterpreneurs Motivation in Self Employment (TEMISE) chini ya mradi ujulikanao kama Hertu Farms, (zinaojihusisha na mafunzo ya ujasiliamali, uendelezaji biashara na  kilimo biashara ikiwemo kilimo cha uyoga, matunda, mboga mboga na ufugaji wa kuku wa kienyeji) zimeendesha mafunzo ya Biashara, masoko, utoaji huduma bora kwa wateja pamoja na kilimo cha uyoga kibiashara, yenye lengo la kuwajengea uwezo wakinamama ili waweze kuboresha biashara zao na  kuzalisha uyoga kibiashara ili waweze kuboresha vipato vyao na hasa kupunguza umaskini.
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyohusisha nadharia na vitendo yalifanyika kuanzia tarehe 6/8/2017 na kumalizika tarehe 9/8/2017, yalifanyika katika kijiji cha Mwanzo Mgumu, Wilaya ya kisarawe, Mkoa wa Pwani. Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo,  ndugu Herman Msagamasi  kutoka HERTU Investment  amesema kuwa utoaji wa mafunzo hayo ni utaratibu waliojiwekea  ambapo kila mwezi hutoa nafasi kwa jamii kujifunza kile taasisi hizo zinafanya, ambapo safari hii waliamua wawajengee uwezo akina mama mbalimbali katika nyanja za Biashara,Masoko,  utoaji wa huduma bora kwa wateja; wakitambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Biashara na hasa namna bora ya kutafuta masoko na kuyahudumia ipasavyo, kwa kutoa huduma bora; pia mafunzo yaliangaziazia kuwafanya wakina mama kuacha kufanya biashara zao kimazoea kama kutoweka kumbukumbu, kutohudumia wateja ipasavyo, kusubiri wateja wawafuate n.k. Pia Mafunzo yalilenga kuwafundisha wakina mama kuzalisha uyoga kama zao la chakula na Biashara; kwa kuzingatia kuwa sekta hii  ya Kilimo cha Uyoga inakuwa kwa kasi nchini ingawa bado hakijapewa umuhimu mkubwa licha ya faida kubwa kiafya, kuingiza kipato na utunzaji wa mazingira.
Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo Ndugu Shaban Kabanga kutoka TEMISE amesema, wajasiliamali wengi wamekuwa wakifanya biashara kwa mazoea na kupelekea kutofikia malengo yao hivyo kupelekea kupoteza muda na rasilimali zao; ameongeza kuwa wajasiliamali wengi wamekuwa wanawekeza kwenye miradi kwa mkumbo, bila ya kufanya utafiti wa kina; anaamini kuwa mafunzo waliyopewa wakina mama hao yatawawezesha  kufanya kufanya ujasilimali mbalimbali kwa ufanisi mkubwa na pia kuzalisha uyoga  kibiashara; ameongeza kuwa; wakina mama  hawajapewa mafunzo ya kuzalisha uyoga pekee kama wanavyofanya wengi bali wamepewa na mbinu za namna ya kufanya Biashara ya kilimo cha uyoga kwa kuzalisha uyoga bora, kufungasha vyema, kupanua wigo wa masoko, na kuhudumia vizuri wateja wao ili kujenga soko kubwa hivyo biashara zao kuwa endelevu. Kwa upande wa washiriki w mafunzo hayo;  Bi. Anna mmoja wa washiriki amesifu namna mafunzo yalivyotolewa kwa kutumia vitendo zaidi kuliko nadharia hivyo imemfanya aelewe zaidi na anaamini  itamsaidia katika kuutekeleza ipasavyo miradi yake na hasa kuanza kilimo cha uyoga. Nae Bi. Sarah akizungumzia mafunzo hayo amesema yamemjenga vilivyo kwani zamani alikuwa anafanya biashara kimazoea mpaka kupelekea kufirisika na kuwa na madeni makubwa;  hivyo kupitia mafunzo hayo amefahamu kosa lake na ataweza kujirekebisha; "pia nimejifunza uyoga ni chakula bora sana kuboresha afya zetu kwa kuwa una viinilishe vingi na ni biashara nzuri sana kwani kilimo chake ni rahisi kwa mtaji, eneo dogo, maji kiasi na huchukua muda mfupi hadi kuvuna na pia unavunwa kipindi chote cha mwaka kwani hautegemei mvua. 
Kwa mujibu wa taasisi hizo, mafunzo kama hayo yanatarajia kufanyika tena tarehe 18.08.2017, jijini Dar es salaam.

Thursday, 3 August 2017




Tumekuwa tukiulizwa na watu wengi sana juu ya soko la uyoga nchini Tanzania. Makala hii inajikita kuelezea hali halisi ya soko la uyoga na biashara kwa ujumla.
Uyoga na mazao yake (bahati mbaya hadi sasa tunazalisha uyoga pekee)  licha ya kuwa na faida kubwa kwa nchi na kwa kipato cha mwanachi mmomoja.Kilimo na  biashara ya uyoga katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ipo chini sana. Kilimo kinafanyika kwa uchahe sana na kiasi kidogo; kwa maana ya kilimo kinafanyika si kibiashara hivyo kutokuleta tija kwa taifa na kwa wakulima.

Soko la uyoga
Je, Uyoga una soko?    Kilimo cha Uyoga kinalipa?
Awali ya yote bidhaa yoyote ili iweze kupata soko, ari, bidii na juhudi kubwa inabidi kufanyika kuanzia katika kuizalisha ili iwe  bora na inayopendwa na wateja;  pia katika kuitengenezea mazingira mazuri ya ya bidhaa hiyo kununulika kama  kuitangaza n.k

Tunasema uyoga una soko kubwa hasa hapa nchini na ni biashara kubwa. Zifuatazo ni hoja kadhaa zinazothibitisha hoja hii.

·     1. Uyoga ni utamaduni wa Mtanzania: Uyoga tangu enzi umekuwa ukitumika kama chakula na dawa kwenye makabila mengi hapa nchini Tanzania. Makabila mengi kipindi cha masika wamekuwa wakivuna uyoga porini  na kuutumia kama mboga au kutibu magonjwa mbalimbali; pia uyoga hukaushwa na kutunzwa kwa matumizi ya baadae. Uvunaji au ukusanyaji wa uyoga huu hukabiliwa na changamoto kadhaa kama; 

(a)  uyoga hupatikana kipindi cha mvua (masika) pekee
(b)  kushambuliwa kwa wavunaji na wadudu au wanyama wakali kama nyoka n.k,
(c)  kuvuna/kukusanya uyoga wenye sumu kimakosa (kuna uyoga unaofaa kuliwa na wenye sumu ambao haufai kuliwa na mwanadamu).
(d)  uharibifu wa mazingira; kuna mahusiano makubwa baina ya uyoga na mazingira endapo; mazingira hayatatunzwa ipasavyo uyoga hautamea/hautapatikana. Hivi sasa uyoga haupatikani kwa wingi kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Hii hoja inadhihirisha kuwa kilimo cha uyoga ni fursa kubwa nchini, uwepo wa teknolojia ya kulima Uyoga inafanya Uyoga upatikane kipindi chote cha mwaka (na kama tafiti zikifanyika kwa wingi aina nyingi za uyoga kutoka porini zitalimwa kwenye mashamba ya uyoga), kupunguza vifo vitokanavyo na ulaji wa uyoga sumu au kushambuliwa na wanyama, na pia kusaidia utunzaji wa mazingira. Endapo wakulima watalima uyoga kibiashara; uyoga ni biashara kubwa na itawezesha kuongeza pato la taifa na kuwa chanzo cha ajira nchini.

2  2. Kubadilika kwa mtindo wa maisha  : kumekuwa na uhamiaji mkubwa wa watu kutoka vijijini kwenda mjini; hii imesababisha ile ari na mwamko wa ulaji wa uyoga kupungua kwani licha ya kuwa na mtu anauhitaji mkubwa kwani alikuwa anaula alipokuwa kijijini. Hii imesababishwa na kutopatikana kwa urahisi uyoga maeneo ya mijini, mtu akihitaji uyoga ni lazima aagize uyoga vijijini. Kutokana na mwamko wa ulaji wa uyoga kushuka imepelekea kizazi kinachofuatia pia kutokuwa na ari na mwamko wa kula uyoga licha ya faida zinazopatikana mwilini.
Mtindo wa maisha  ni pamoja na ulaji, ulaji kwa miaka ya hivi karibuni umebadilika kutokana na sababu mbalimbali  watu sasa wameacha au kupunguza  kula vyakula vya asili na kupendelea kula vyakula vya kisasa.

·      3. kuwepo kwa wageni kutoka nchi mbalimbali; baadhi ya nchi ulaji wa uyoga ni utamaduni unaoendelezwa, kutokana na faida za kilishe zinazopatikana kwenye uyoga, hivyo wanapokuwa hapa nchini hupendelea kuendelea na utamaduni wao. Kumekuwa na migahawa mingi nchini inayopika vyakula mahsusi kutokana na utamaduni wa taifa fulani, mfano migaawa ya kichina, kifaransa, kijerumani n.k
·          Uwepo wa mahoteli, migahawa (restaurants), maduka makubwa ya vyakula na vitu vingine (supermarkets); hoteli na maduka makubwa ni sehemu zenye uhitaji mkubwa wa bidhaa hasa za kilimo na Uyoga ukiwemo.

·       4. itaji mkubwa wa uyoga unaolimwa au kupatikana ukanda wa afrika; mataifa mbalimbali ya ulaya yanaamini nchi zinazoendelea hasa za afrika bado mazingira hayajachafuliwa sana kulinganisha na nchi zao. Hivyo mataifa hayo hupendelea bidhaa nyingi hasa za kilimo ukiwemo uyoga kutoka ukanda wetu wan chi za kiafrika; ingawa bado uyoga haujapewa kipaumbele kama mazao mengine ya kilimo.

·      5. wamko mdogo wa kulima uyoga: Nchini Tanzania na nchi zingine za kiafrika kilimo cha uyoga bado hakijatiliwa mkazo licha ya kuwa ni na faida kubwa kiafya, kiuchumi na kimazingira. Ni wakulima wachache sana wanaojihusisha na kilimo cha Uyoga kibiashara licha ya uhitaji mkubwa wa uyoga.
·       6. Kutokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha hasa ulaji mbaya wa chakula kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo la moyo, matatizo ya figo n.k; wagonjwa wenye magonjwa hushauriwa kula uyoga. Pia kumekuwepo na mwamko mkubwa wa jamii juu ya ulaji wa vyakula vya asili (organic food) ikiwemo Uyoga hivyo ulaji na mahitaji ya Uyoga yanaongezeka siku hadi siku.
 
Mwisho:Kutokana na sababu tajwa na sababu nyingine nyingi tunathubutu kusema kuwa uyoga una soko kubwa na ni fursa mpya na yenye uwezo wa kuleta kipato kwa mkulima au mfanyabiashara wa uyoga na bidhaa zake na cha zaidi kuliingizia taifa pato kubwa. Ni sekta kubwa inayokuwa kwa kasi na endapo watanzania tutachangamkia fursa hii kwanza tutaimarisha afya za wananchi na kukuza uchumi wa nchi.
Moja ya changamoto kubwa katika kilimo cha uyoga ni upatikanaji wa Mbegu bora; kwa kuliona hilo HERTU INVESTMENT kupitia mradi wake wa HERTU Farms tunawaletea mbegu bora za Uyoga aina ya Mamama/Oyster mushrooms (nyeupe, pinki na grey), ukiweka oda baada ya siku 14 (wiki mbili) mbegu zinakuwa tayari. Bei ni Tsh. 3,000 kwa chupa.
Unaweza kupiga simu 0783182632/0713600915; Barua pepe hertufarms@yahoo.com au kwa njia ya Whatsup 0757315931

Tunasafirisha mikoa mbalimbali Tanzania na nchi jirani

Pia tunatoa Mafunzo, ushauri, uanzishaji, usimamizi na tathmini ya miradi ya kilimo cha Uyoga kibiashara.
Tunapatikana Mwananyamala-komakoma, Biashara complex, Ghorofa ya 3, Ofisi #301; pia shambani Kisarawe-Mwanzomgumu, Mkoa wa Pwani.

KARIBU KATIKA SEKTA HII MPYA INAYOKUA KWA KASI NCHINI; KWA KUIMARISHA AFYA, KIPATO NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

#MabadilikoniLazima
Pinki
Hudhurungi (Grey)
Nyeupe




 
Banda/Shamba la kuoteshea uyoga linajengwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana kwenye mazingira yako. Sehemu za joto linaweza kujengewa nyasi na udongo, matete, Makuti n.k. ili kuhifadhi ubaridi na sehemu za joto hata tofali na bati unaweza kujengewa.

SIFA ZA BANDA
1. Liwe na uwezo wa kuhifadhi unyevu nyevu na ubaridi
2. Liwe na uwezo wa kuzuia wadudu na wanyama waharibifu kama panya,jongoo,konokono, pia inzi n.k
3. Liwe na mzunguko mzuri wa hewa n mwanga wa kutosha hasa wakati wa kuotesha; isipokuwa wakati wa utandaji wa mbegu mifuko ya uyoga unahitaji giza kiasi
4. Banda lisijengwe karibu na jalala la takataka, mabanda ya wanyama kama kuku,ng'ombe n.k
4. Lisiruhusu jua kuingia na upepo mkali
5. Liwe safi muda wote.
Kwa ushauri na mafunzo juu ya #KilimochauyogaKibiashara wasiliana na wataalamu waliobobea kwa namba 0783182632/0713600915 pia unaweza kufika Mwananyamala-Komakoma, Jengo la Biashara Complex, Ghorofa ya 3,Ofisi #301.
#UyogakwaAfyaKipatoMazingira

 #MabadilikoniLazima
Tumia maarifa, vipawa, rasilimali, muda na chochote ulichonacho kuhakikisha ndoto yako inatimia, ili uweze kutathmini, kama inafaa uweze kupanua wigo wa ndoto yako; huwezi kujua kama ndoto yako ni bora au sio mpaka uifanyie kazi mpaka mwisho; usiguse jambo au biashara ya ndoto yako na kuacha kabla hakijatimia wengi tumekuwa tukitaka kufanya mengi na kuacha bila ya kukamilisha hapo unakuwa unapoteza muda na rasilimali zako na hutofanikisha ndoto zako. Fanya tafiti wa kina katika ndoto yako na ukiona ina tija itekeleze kwa nguvu zako zote mpaka itimie.


About our customers

About our customers

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget