Ukulima wa uyoga ni kitega uchumi kinachoweza kumnasua Mkulima mapema kutoka kwenye u maskini;
1. Ukuaji wake ni wa haraka huchukua takriban siku 30-40 kuanza kuvunwa tangu Mbegu kupandwa. Hivyo hurudisha pesa haraka kwa mwekezaji, na baada ya kuanza kuvunwa mkulima akitunza vizuri ataendelea kuvuna kwa miezi 2 hadi 4, kwa mpando mmoja
2. Huhitaji eneo dogo la ardhi
3.Gharama za uendeshaji ni ndogo sana haihitaji umeme, hutumia masalia ya mazao na takataka kuzalishia uyoga n.k (gharama kubwa hutumika kwa miundombinu ya awali kama mashamba na vifaa n.k)
4.Hautegemei misimu ya mvua; hivyo Mkulima hujipatia kipato chake kipindi chote cha mwaka tofauti na mazao mengine.
BAADA YA KUVUNA
5.Mabaki baada ya uyoga kuvunwa hutumika kama mbolea nzuri na ya Asili kwa kuoteshea mimea kama matunda na mboga mboga; pia hutumika Kutengeneza chakula cha mifugo.
Lakini ili kuwa na kitega uchumi cha uhakika zaidi mtu yoyote anayetaka kuwekeza kwenye sekta hii hana budi kujifunza vizuri, na kwa undani sayansi na teknlojia ya ukulima wa aina mbalimbali za Uyoga: Uyoga wenye soko la uhakika, Uyoga wenye manufaa katika kuboresha afya ya jamii.
Imetolewa katika kitabu cha "UYOGA, FAIDA ZAKE KU-AFYA, KI-UCHUMI, KI-MAZINGIRA, NA KATIKA UKULIMA WAKE"; Keto E. Mshingeni, PH.D
Profesa, Hubert Kairuki Memorial University