
Majibu ya mitazamo hiyo ni kama ifuatavyo.
Kuna aina nyingi za
kuvu(fungi) duniani, inakadiriwa zipo aina milioni moja na nusu za fungi /kuvu, aina 64,000 tu ndio zimefanyiwa utafiti na wanasayansi duniani, na
kati za hizo aina 10,000-12,000 zinaweza kutoa uyoga lakini aina 2,000 za uyoga
ndizo zinazotumika kwa chakula, uyoga mwingine hutumika kama dawa za kutibu
maradhi mbali mbali.
Ili kuepuka baadhi ya
athari za baadhi ya uyoga wenye sumu hasa ule wa porini, wataalamu walifanya utafiti wa uyoga ili
kupata uyoga usio na sumu na wenye virutubisho zaidi na unaoweza kutumia kama lishe
na dawa;Ili kuepuka athari za baadhi ya uyoga sumu ambazo kwa kiasi kikubwa
zinatokana na kutoutofautisha au kufananisha uyoga pori unaofanana na unaoliwa
ni vizuri kulima uyoga kwa kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti; utafiti huu
umfanywa kwa kutambua tu aina ya uyoga tu na haujafanyiwa mabadiliko yoyote ya
kibailogia); na wengi hawajui kuwa uyoga pori ndio chanzo cha vijikuvu(mycelia)
vinavyotumika katika utengenezaji wa mbegu za uyoga unaolimwa; na uyoga
unaolimwa hauwezi kamwe kubadilika na kuwa sumu.
Dhana nzima ya kukusanya
uyoga pori ni budi uendelee kwa kufuata kanuni kadhaa ambazo zimerithishwa
kutoka kizazi na kizazi au kwa njia za utafiti wa kisayansi ambazo
zinahakikisha kuwa uyoga unaovunwa hauna sumu. pia juhudi za utunzaji wa
mazingira uendelezwe ili uyoga uendelee kupatikana kwenye mazingira yetu. na
hapa nchini Tanzania wataalamu/watafiti wafanye tafiti nyingi ili tuweze kulima
uyoga aina nyingi kutoka kwenye mapori yetu, kwani Tanzania tuna utajiri wa
aina nyingi za uyoga ambazo zinaweza kutumika kama dawa na tiba.
Kinachofanyika ni kuwa
baada ya kufanya utafiti wa mbegu pia utafiti ulifanywa juu ya mazingira ambayo
uyoga pori huota kwa maana ya kwenye vichuguu,chini ya miti na kwenye
miti/magogo; uyoga huota huko kwa sababu ya mazingira yana chakula/viinilishe
ambao uyoga kama mmea hupata chakula chake kwani hauwezi kujitengezea chakula
chake kwa njia ya usanisi wa chakula (photosynthesis) yaani kutumia umbijani
(chlorophyll). Hivyo tunalima uyoga kwa kutengeneza mazingira yaleyale
yanayohitajika uyoga kuoata; tunatumia masalia ya mazao kama maganda ya
alizeti, karanga nk majani ya mpunga, ngano; maranda ya mbao ngumu na lakini
zisizo na dawa, mabaki ya miwa,pamba nk; Tunajenga nyumba za udongo na kuuzeka
na nyasi sehemu zenye joto (sehemu za
baridi haziitaji nyumba za udongo na nyasi) ili kuhifadhi unyevu nyevu na
baridi kama kwenye kivuli cha miti na kwenye vichuguu, na hii ili kufanya uyoga
huu uwe unalimwa kipindi chote cha mwaka tofauti na wa porini ambao unapatikana
kipindi cha masika tu.
Hivyo kama nchi
ingewekeza kwenye utafiti wa huu uyoga pori ungeweza kulimwa au kuyalinda
mazingira na kupatikana kipindi chote cha mwaka na tungeweza kuimarisha afya na
kupunguza utapiamlo nchini na hata kujenga viwanda vya dawa nk; kwa nchi za
wenzetu uyoga na mazao yake ni biashara kubwa sana duniani. Na kwa taarifa tu Uyoga
pori huu huu unaopatikana kuna wazungu wanakuja wanafanya utafiti wao na
kuupeleka kwenye soko la dunia na kuuza kwa fedha nyingi sana.

Kutokana na uharibifu wa mazingira, watu wengi kuhama kuja mijini na kupotea kwa utamaduni wa kula uyoga utamaduni wa kula uyoga umepotea na kutokuwa na tafiti nyingi za kuendeleza upatikanaji wa Uyoga ule wa pori kama nchi zingine; uyoga umepoteza umaarufu licha ya kuwa ni biashara kubwa duniani na ni chanzo cha lishe nzuri kutokanana virutubisho vyake Pia Uyoga una nafasi ya kuwa chanzo cha ajira ili kukuza kipato, kukuza pato la taifa na kutunza mazingira kwa kutumia masalia ya mazao mbalimbali kuzalisha uyoga.
Herman Msagamasi
Founder&MD
HERTU Investement (HERTU Farms Project)
Cell: +255783182632
Whatsup: +255757315931
Instagram/Twitter: @hertufarms
Blog: hertufarmsblogsport.com
0 comments:
Post a Comment