Katika kuadhimisha siku muhimu ya Mama Duniani (Mother's Day) HERTU Investment/ Hertu Farms na Temise Tanzania ambao moja ya malengo yao wamejikita katika kumkomboa mwanamke hasa kiuchumi, tukiamini kuwa mwanamke kumiliki uchumi wake ni moja ya fursa kubwa kwake kuweza kujiwezesha na zaidi kuleta chachu kubwa katika ustawi wa uchumi jamii na taifa kwa ujumla. Tumekuwa tukitoa mafunzo ya ujasiliamali, Biashara na Masoko na Kilimo cha uyoga na tukilenga zaidi kina mama na vijana. Kwa muda sasa tumekuwa na kikundi cha wakina mama kijulikanacho kama #Wachapakazi ambapo tumewapa mafunzo ya namna bora ya kujiendesha, Biashara, Masoko, utoaji wa huduma bora kwa wateja, uaandaji wa mipango biashara, uanzishwaji na usimamiaji wa miradi, ambapo moja ya mradi waliojifunza ni Kilimo cha Uyoga kibiashara.
Kwa kutambua ari kubwa, hamasa, juhudi zao, na kujituma kwao katika kutimiza ndoto na matarajio yao na kutambua umuhimu wa mwanamke katika jamii hasa kiuchumi. Tunapenda kutangaza rasmi kuwa Kikundi hiki cha #WACHAPAKAZI chenye makao yake makuu, Mtaa wa Mafichoni, Manzese Dar es Salaam, kiitakuwa sehemu ya wana #MabadilikoniLazima. Na kuanzia leo ndio watakao kuwa na jukumu la kuzalisha Uyoga na bidhaa zake shambani Hertu Farms lililopo Kijiji cha Videte, MwanzoMgumu, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani.
Hivyo tunaomba wadau wetu, na jamii kwa ujumla na hasa wadau wa Maendeleo kuwapa ushirikiano wa hali na mali kama kununua bidhaa zao, mawazo na hata kuwawezesha zaidi kiuchumi ili watimize malengo yao mengi walionayo. Tunafaraja kubwa kuoana kuwa nyuma ya bidhaa za Hertu Farms kuna Nguvu kubwa ya wakina Mama #Wachapakazi.
Nauli mbiu ya Wachapakazi: "Kazi ni Kazi daima, mwiko kukata tamaa"
HAPPY MORHERS' DAY
Imetolewa na
Shaban Kabanga
Meneja Miradi
HERTU Investment (Hertu Farms)
Simu:0713600915
Whatsup: 0712047com
E-Mail: Shabankabz@yahoo.com
Blog: hertufarms.blogsport.com